Mazingira Yetu

Naturalliance network huendeshwa na 

Umoja wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN), kukusaidia kuishi vyema. Kuishi vyema unahitaji kufanya uwamuzi wa busara, kwako na kwa jamii yako,kuhusu manufaa na hatari kutokana na dunia asili. IUCN hukubali maarifa kutoka kwa mashirika 1400, ikiwemo serekali 90 na wataalamu 24,000 kutoa ujuzi mzuri zaidi kwa uamuzi kuhusu dunia asili.

 
Zingatia COVID-19 kwa makini
16 Feb 2022

Tafadhali zingatia kwa makini kuhusu tishio kwenu na kwa mazingira kutokana na COVID-19. Tumia mwaidha yanayotoka tu kwa mashirika yanayoaminika kuhusu jinsi wewe na jamii yako mnaweza kutambua na avoid kuzuia ugonjwa huu . Virusi hivi hunawiri katika hewa nyevu na tunaambukizwa kupitia kinywa, pua na macho. Kwa hivyo ushauri muhimu ni:

  • Weka umbali wa mita 2 na watu – epuka hewa wanayopumua nje;
  • vaa barakoa unapozingirwa na watu wengi katika sehemu finyu au katika makundi; 
  • zingatia sheria kuhusu kusafiri na upate chanjo ukiweza;

 

Hatua dhidi ya mikurupuko ya usoni lazima pia  ipatikane kwa busara , kwa misingi ya  sayansi nzuri zaidi  . Sheria mpya lazima  isilete madhara kwa maisha mashinani na kwa uhifadhi wa mazingira  .

 

Tunaishi katika dunia iliyoshawishika sana na binadamu, lakini haikuwa hivyo kwa kawaida. Binadamu wa kisasa walibadilika kwa millennia nyingi kama vikundi vidogo vya wawindaji - watafutaji. Mababu zetu waliwinda, walivua na walitafuta mazao ya mimea kabla ya kujifunza jinsi ya kukuza mimeana kufuga wanyama. Hii ilileta aina ya viumbe kwa njia tusizoelewa kikamilifu.

 

Michoro katika mapango inaashiria kwamba heshima kwa wanyama wengine imekuwa muhimu tangu. Uwindanji ulileta uhifadhi wa kwanza wa mazingira na wavuvi kupanga kurejesha mito. Mashirika ya kulinda wanyama yalianzishwa na watu waliowahurumia wanyama waliohitaji wenzao.

 

Siku hizi, binaadamu hutawala na kudhuru utajiri wa mazingira. Ilhali  sote tunategemea mazingira  kwa hewa tupumue, maji safi, na hali nzuri ya hewa kukuza mimea. Wengi wetu wana afya kupitia kufurahia mazingira. Lazima tujifunze njia  za kusimamia mazingira vizuri , angalau kwa COVID-19 na biashara ya wanyamapori . Kama unafurahia chakula cha mwituni au unapenda tu kutazama wanyamapori, wewe pia unaweza kusaidia kuhifadhi rasilimali hizo.

 

Wawindaji na watazama wanyama huwa hawashirikiani, lakini wanahitaji kushirikiana. Migogoro huondoa ufuatilizi wa hatari kwa kila kitu, kama vile  mabadiliko yamazingira . Kutumia rasilimali inayoweza kutumika kwa muda mrefu haina tofauti na kutumia mazao yaliyolimwa, lakini ni nzuri zaidi kwa kuhifadhi mazingira. Uwindaji, ukulima na matumizi mengine ya raslimali asili vinaweza kuwa suluhisho kwa uhifadhi na tishio kutokana na ongezeko la joto duniani. Tunahitaji kuzingatia kwa pamoja kuleta suluhisho, inayotokana na teknolojia inayoleta maisha mapya na inayotokana na mazingira yenyewe.